Mkurungezi Mkuu ZBC Atenguliwa

0
144

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Zanzibar (ZBC) Dkt. Saleh Yussuf Mnemo.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya Habari na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar Mhandisi Zena Ahmed Said imesema uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu huyo umetenguliwa kuanzia hii leo.