Sehemu ya jengo la Bunge la Afrika Kusini lililopo mjini Cape Town limeungua moto.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Afrika Kusini, Moto huo ulianza kwenye paa la ghorofa ya tatu ya jengo hilo.
Ajali hiyo ya moto imetokea saa chache baada ya mazishi ya Askofu Mkuu Desmond Tutu katika Kanisa Kuu la St George lililopo karibu na bunge.
Hakuna taarifa za mtu yeyote kupata madhara ya moto huo uliozuka wakati huu ambapo watumishi wakiendelea na mapumziko ya mwanzo wa mwaka.
Chanzo cha moto huo bado hakijafahamika lakini uchunguzi unaendelea na tayari mtu mmoja amekamatwa na kuhojiwa kutokana na tukio hilo.
Jengo hilo lina sehemu tatu zilizosheheni historia ya Afrika Kusini ambapo jengo la zamani zaidi lilijengwa mwaka 1884.