Rangi wa mwaka 2022 – Pantone 17-3938 “Very Peri”

0
209

Kila mwaka mamlaka ya kimataifa ya rangi – Pantone huchagua rangi ya mwaka na kwa mwaka 2022 rangi ya ‘Veri Peri’ imechaguliwa kuwa rangi ya mwaka

Kampuni hiyo inafafanua ‘Very Peri’ kama rangi inayonyumbulika na inayobadilika katika matumizi yake, ni rangi yenye bluu ya ‘periwinkle’ ambayo ina urujuani yenye chembe chembe za rangi nyekundu ‘violet red’ ambayo huwa urujuani inayong’aa iliyochanganywa kuleta tunu za uaminifu, uthabiti na uthubutu kutokana na msisimko wa rangi nyekundu.

Ili kufikia uteuzi wa rangi kila mwaka, wataalam wa Pantone huchagua rangi ya mwaka kwa kuchunguza athari za rangi duniani kote, kutoka sehemu mbalimbali kama vile tasnia ya burudani na filamu katika uzalishaji, makusanyo ya Sanaa za kuchora, wasanii wapya, mitindo, vyombo vya nyumbani, maeneo ya kubuni, maeneo maarufu ya kusafiri, pamoja na maisha mapya, michezo, hali ya kijamii na kiuchumi

Vilevile uteuzi huzingatia ushawishi unaotokana na teknolojia mpya, nyenzo, maumbo na madoido yanayoathiri rangi, mifumo husika ya mitandao ya kijamii na hata matukio yajayo ya michezo yanayovutia watu duniani kote.

Kwa miaka 23, Rangi ya Mwaka ya Pantone imeathiri ukuzaji wa bidhaa na maamuzi ya ununuzi katika tasnia nyingi, ikijumuisha mitindo, vifaa vya nyumbani, na muundo wa viwandani, pamoja na ufungaji wa bidhaa na muundo wa picha.