Karagwe wakamilisha ujenzi wa madarasa kwa zaidi ya asilimia 95

0
144

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa amewapongeza viongozi mbalimbali wilayani Karagwe mkoani Kagera, kwa kusimamia vizuri matumizi ya shilingi bilioni 1.7 zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya kuboresha sekta ya elimu.

Waziri Bashungwa ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Karagwe ametoa pongezi hizo kufuatia kukamilika kwa ujenzi wa vyumba 80 vya madarasa kwa zaidi ya asilimia 95 wilayani humo.

Ametoa pongezi hizo akiwa katika kata ya Chonyonyo baada ya kujionea kazi ya ujenzi wa vyumba hivyo vya madarasa iliyofanywa kwa ushirikiano baina ya Viongozi wa ngazi za shina, vijiji, kata, wilaya pamoja na Wananchi.

Waziri Bashungwa pia ameishukuru Serikali kwa kutoa fedha kwa ajili ya kujenga na kuboresha miundombinu mbalimbali wilayani Karagwe pamoja na kufadhili miradi mbalimbali ya maendeleo.