Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameuagiza uongozi wa mkoa wa Ruvuma kuhakikisha kila Halmashauri inajenga vyumba vya madarasa vya kutosha ili kuwawezesha wanafunzi waliofaulu kwenda kidato cha kwanza wanapata nafasi za kuendelea na masomo yao.
Agizo hilo amelitoa baada ya kusomewa taarifa ya miradi ya maendeleo ya mkoa wa Ruvuma na Mkuu wa mkoa huo Christina Mndeme.
Waziri Mkuu amesema watoto wote waliofaulu lazima wahakikishe wanasoma hivyo waweke nguvu katika ujenzi wa vyumba vipya vya madarasa.
Katika hatua nyingine Waziri Mkuu Majaliwa amesema serikali inaendelea na mpango wa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami barabara zote zinazounganisha mkoa kwa mkoa na wilaya kwa wilaya.
