Rais Samia: Tusherehekee kwa amani na utulivu

0
152

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kupitia ukurasa wake wa Twitter ametuma salamu na kuwatakia heri ya Sikukuu ya Krismasi na mwaka Mpya kwa watanzania wote huku akiwasihi kusheherekea Sikukuu hizo kwa furaha, amani, utulivu na kiasi

Aidha Rais Samia Suluhu Hassan amewataka watanzania kuendelea kuwa na umoja kuelekea mwaka mpya wa 2022 huku wakichapakazi kwa weledi wa hali ya juu, uzalendo na nidhamu ili kupiga hatua mbele zaidi kimaendeleo

Kila mwaka ifikapo tarehe 25 mwezi Desemba Wakristo kote duniani huadhimisha Sikukuu ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo miaka zaidi ya 2000 iliyopita sambamba na mataifa mengi duniani kusheherekea Sikukuu ya kuanza mwaka mpya ifikapo tarehe mosi Januari.

TBCOnlineUpDate