Watu Mashuhuri ambao wamefariki lakini kurasa zao za Instagram zipo hai

0
2896

Michael Jackson

Mfalme wa Pop aliyekuwa maarufu kwa nyimbo zake za “Thriller” na “Billie Jean,” na hajaacha kutusisimua na sauti yake kwenye nyimbo zake hadi leo

Ingawa Michael Jackson aliaga dunia mwaka wa 2009, Ukurasa wake Instagram sasa unafuatwa na wafuasi Milioni 6.6.

Marilyn Monroe

Marilyn Monroe ni Muigizaji wa Marekani na alifariki mwaka 1962, ukurasa wa Instagram wa Marilyn ni @marilynmonroe. Hupostiwa picha za zamani, filamu zake za Hollywood na hadithi zake.

Watu wanampenda sana, na hutumia hashtag #MarilynMonroe na ukurasa wake wa Instagram una wafuasi Milioni 1.7.

Whitney Houston

Alipendwa kwa nyimbo zake nyingi lakini hizi ndo kiboko yao “I Will Always Love You” na ” I Have Nothing” vibao hivi vimemfanya Whitney Houston kuwa mwanamuziki wa kimataifa

Akaunti yake rasmi ya Instagram huhifadhi kumbukumbu za uhai wake kwa kupostiwa picha na video zake pambe mpaka sasa ana wafuasi 698,000. Whitney Houston amefariki mwaka 2012

Elvis Presley

Wimbo wake wa “Can’t Help Falling in Love” ni mojawapo ya nyimbo zilizofanikiwa sana katika historia ya muziki na akawa mfalme wa Rock ‘n’ Roll. Elvis Presley aliaga dunia Memphis mwaka wa 1977.

Kwenye Instagram, mashabiki wanaweza kuona picha ambazo hazijachapishwa na maudhui adimu Elvis Presley na ina wafuasi Milioni 1.2

Tupac Amaru Shakur


Tupac Amaru Shakur alizaliwa 16 Juni 1971 na kufariki 13 Septemba 1996, alikuwa mwigizaji, mwanaharakati wa haki za binadamu, na pia mwanamuziki maarufu wa muziki wa hip hop kutoka nchini Marekani.

Anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama 2Pac. Ni mmoja kati ya wasanii wa hip hop waliouza rekodi nyingi za muziki dunia. Huyu alikuwa mtoto wa Afeni Shakur, ambaye alikuwa mwanachama wa chama cha Black Panther Party.

Mama yake Tupac alitolewa jela mwezi mmoja kabla ya kuzaliwa Tupac. Tupac alikufa mnamo tar. 13 Septemba katika mwaka wa 1996 baada ya kupigwa risasi akiwa anaendesha gari mjini Las Vegas, Nevada.

Pamoja na kufariki lakini kuna akaunti ya Instagram inayotumia jina lake lenye wafuasi milioni 6.3.

Robert Nesta Marley

Jina lake kamili ni Robert Nesta Marley, baadae aliamua kujiita Bob Marley.

Bob Marley alizaliwa tarehe 6 February ya mwaka 1945 katika vijiji vya Nile Mile katika parish ya mtakatifu Ann huko Jamaica.

Baba yake alikuwa anaitwa Norvan Sinclair Marley ambaye alikuwa mzungu na mama yake anaeitwa Cedela Booker ambae ni mjamaica mweusi.

Historia ya maisha yake haina tofauti sana na wanamuziki wengine wa Reggae ambao walikuwa marafiki zake kama Peter Tosh aliyelelewa na shangazi yake, Burning Wailer aliyelelewa na baba yake zaidi.
Bob Marley yeye alilelewa na mzazi mmoja (ambae ni mama yake) pale alipofiwa na baba akiwa na umri wa miaka kumi tu.

Pamoja na kutokuwepo duniani lakini upo ukurasa wa Instagram unaotumia jina lake ukiwa na wafuasi milioni 6.2