Askari mmoja wa kike wa jeshi la Nigeria amekamatwa kwa madai ya kukubali ombi kuolewa akiwa kazini.

0
149

Habari kutoka nchini Nigeria zinaeleza kuwa askari huyo amekiuka maadili ya kijeshi kwa kufanya vitendo vilivyo kinyume na maadili akiwa amevaa sare za jeshi.

Picha za video zimesambaa katika mitandao ya kijamii nchini Nigeria zikimuonesha askari huyo akiwa anavalishwa pete ya uchumba, tukio lililoshuhudiwa na kushangiliwa na watu mbalimbali.

Baadhi ya wanaharakati wa kutetea haki za Wanawake nchini humo limelishutumu jeshi la Nigeria kwa hatua yake ya kumkamata askari huyo wa kike kwa kile walichodai kuwa ni ubaguzi.

Wamedai kuwa hatua kama hizo zimekuwa hazichukuliwi kwa askari wa kiume ambao wamekuwa wakionesha hadharani vitendo kama hivyo wakiwa wamevalia sare za kijeshi.