Rais Samia ateta na Walimu kwa njia ya simu

0
180

Rais Samia Suluhu Hassan amewataka Walimu nchini kuendelea kufanya kazi kwa bidii, kwa kuwa Serikali inatambua madai yao na inayafanyia kazi.

Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo wakati akizungumza kwa njia ya simu na Wakuu wa shule za sekondari wanaohudhuria mkutano mkuu wa
wakuu wa shule za sekondari za Serikali na zile za binafsi, mkutano unaofanyika mkoani Dar es Salaam.

Amewaeleza Walimu wanaohudhuria mkutano huo kuwa, kutokana na
majukumu mengi ya kikazi ameshindwa kuhudhuria mkutano huo,
lakini anaufatilia kwa karibu na yupo pamoja nao.

Mkutano huo wa 16 unawakutanisha wakuu hao wa shule ili waweze
kubadilishana mawazo, uzoefu pamoja na kujadili changamoto na mafanikio katika eneo lao, na unahudhuriwa na Walimu zaidi ya elfu tano kutoka shule za sekondari za Serikali na zile za binafsi.