Liverpool yazidi kuikaba koo Man City

0
111

Mohamed Salah usiku wa kuamkia leo amefunga bao lake la 22 tangu kuanza kwa msimu huu, baada ya kuiwezesha timu yake ya Liverpool kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Newcastle United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.

Liverpool imeshuka dimbani bila walinzi wake wawili wa kati Virgil van Dijk na Fabinho kutokana na kupatikana na ugonjwa UVIKO -19, lakini wamefanikiwa kupunguza tofauti ya alama baina yao na vinara wa ligi hiyo Manchester City.

Diogo Jota aliisawazishia Liverpool bao ambalo pia lililalamikiwa na wachezaji wa Newcastle, wakidai mchezaji wao mmoja alikua ameumizwa na ilipaswa kuwe na mchezo wa kiungwana (Fair Play).

Baada ya bao hilo, Liverpool ikawasha moto na dakika nne baadaye wakapata bao la pili kupitia nyota wake raia wa Misri Mohamed Salah ambaye alimalizia mpira uliomshinda mlinda mlango wa Newcastle, Dubravka.

Bao la tatu la Liverpool limefungwa dakika ya 87 na Tent Alexander- Arnold baada ya kumalizia vema pasi ya Firmino