Kampuni za upelelezi zapigwa stop Facebook

0
147

Mtandao wa Facebook ambao umebadili jina na kujiita Meta, umepiga marufuku kampuni saba ambazo zimekuwa zikikodiwa kuchunguza taarifa za watumiaji wa mtandao huo.

Kwa mujibu wa mtandao huo, wateja elfu 50 watapewa onyo kuhusu matumizi mabaya ikiwemo vitendo vya upelelezi ambapo baadhi yao wamekuwa wakifungua akauti bandia na kuanzisha mijadala yenye lengo la kukusanya taarifa za kijasusi.

Miongoni mwa makundi yanayolengwa katika ukusanyaji wa taarifa zao kwa kutumia njia za kijasusi ni waandishi wa habari na makundi ya wanaharakati wa haki za binadamu.

Taarifa ya uchunguzi kuhusu suala hilo imeonesha kuwa wapelelezi hao wamelenga watu kutoka zaidi ya nchi mia moja kupitia mitandao ya Facebook, Instagram na Whatsapp.