Waziri wa Maji Jumaa Aweso amemsimamisha kazi Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira mjini Mpanda mkoani Katavi (MUWASA) Mhandisi Mikaya Gimbi, kwa madai ya kushindwa kusimamia utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa tenki la maji la Mapinduzi, lililojengwa kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni 560.
Waziri Aweso amefikia uamuzi huo ikiwa ni miezi miwili tangu kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka huu Josephine Mwambashi kukataa kuzindua mradi huo kwa madai kuwa ulitekelezwa chini ya kiwango.
Amesema pamoja na kushindwa kusimamia mradi huo wa maji, pia Kaimu Mkurugenzi huyo wa MUWASA ameshindwa kusimamia mamlaka yake iweze kujiendesha na kushindwa kulipa madai ya wazabuni pamoja na watumishi.
Aidha Waziri Aweso ameagiza Mkandarasi Millenium Master Builder aliyetekeleza mradi huo wa ujenzi wa tenki la maji wa Mapinduzi kujisalimisha kwenye ofisi za MUWASA ili kujibu tuhuma zinazomkabili.
Kuhusu aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira mjini Mpanda mhandisi Zakaria Nyanda ambaye amestaafu, Waziri Aweso ameagiza afike mkoani Katavi ili kusaidia kutoa maelezo ya kina juu ya utekelezaji wa mradi huo.
Waziri wa Maji Juma Aweso, amemsimamisha kazi Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Mjini Mpanda-MUWASA, Mhandisi Mikaya Gimbi, kwa madai ya kushindwa kusimamia utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa Tenki la Maji la Mapinduzi mjini Mpanda lililojengwa kwa gharama ya zaidi ya shilingi Milioni 560.
Aweso amelazimika kumsimamisha Kaimu Mkurugenzi huyo, ikiwa ni miezi miwili tangu Kiongozi wa Mbio za Mwenge maalum wa Uhuru Josephine Mwambashi, kukataa kuzindua mradi huo kwa kuwa ulitekelezwa Chini ya kiwango, kwa kutolingana na fedha za serikali zilizowekezwa katika mradi huo.
Amesema Pamoja na kushindwa kusimamia mradi huo wa maji pia Kaimu Mkurugenzi huyo, ameshindwa kusimamia Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira-MUWASA na kushindwa kujiendesha, haiwezi kulipa madai ya wazabuni na watumishi wa Mamlaka hayo.
Aidha ameagiza Mkandarasi MILLENIAM MASTER BUILDER aliyetekeleza mradi huo wa ujenzi wa Tenki la Maji wa Mapinduzi kujisalimisha ofisi za Mamlaka ili kujibu tuhuma zinazo mkabili.
Pia ameagiza aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safii na usafi wa mazingira Mjini Mpanda mhandisi Zakaria Nyanda ambaye amestaafu afike Mkoani Katavi ili kusaidia kutoa maelezo ya kina juu ya utekelezaji wa mradi huo.