Wafundwa kabla ya mashindano ya Taifa Cup 2021

0
2559

Wasanii chipukizi kutoka mikoa mbalimbali nchini inayoshiriki mashindano ya sanaa za maonesho ya muziki wa singeli na kizazi kipya kwenye mashindano ya kombe la Taifa (Taifa Cup 2021), wametakiwa kuwa na nidhamu katika safari yao ya kimuziki.

Rai hiyo imetolewa mkoani Dar es Salaam na Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Zanzibar, Omar Abdalla na Mwasiti Almas ambaye ni mwanamuziki wa Bongo Fleva pamoja na mtayarishaji nguli wa muziki hapa nchini Kimambo Beats wakati wa mafunzo kuhusu sanaa wanayoifanya, mafunzo yaliyofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo Mwasiti amewaeleza wasanii hao kuwa ili waweze kuwa na mafanikio makubwa ni vizuri wakawa na heshima, jambo ambalo amesisitiza kuwa ndio siri kubwa ya mafanikio.

Wasanii hao chipukizi kutoka mikoa mbalimbali nchini inayoshiriki mashindano ya sanaa za maonesho ya muziki wa singeli na kizazi kipya kwenye mashindano ya kombe la Taifa, watachuana hii leo kumtafuta mkali wa Singeli, R&B na Hip Hop.