Rufaa ya kina Sabaya kuanza kusikilizwa Februari

0
192

Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Arusha imepanga kuanza kusikiliza rufaa iliyofunguliwa na aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili Februari 14 mwaka 2022.

Sabaya kupitia Mawakili wake wamekata rufaa kupinga hukumu iliyotolewa Oktoba 15 mwaka huu, na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.

Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Arusha, Ruth Massam amesema kuwa, leo rufaa hiyo ilipangwa kwa ajili ya kutajwa na kupangiwa tarehe ya kuanza kusikilizwa.

Amesema rufaa hiyo itaanza kusikilizwa mfulululizo mbele ya Jaji atakayepangwa.

Oktoba 15 mwaka huu, Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Odira Amworo aliwahukumu Sabaya na wenzake wawili kifungo cha miaka 30 jela kila mmoja baada ya kukutwa na hatia katika makosa matatu, ikiwamo unyang’anyi wa kutumia silaha.