Tanzania yang’ara Tuzo za AFRIMMA 2021

0
2447

Mwanamuziki wa Bongo Flava Nassib Abdul maarufu Diamond Platnumz ameibuka kidedea kwa kuwa Mwanamuziki bora wa kiume kwa Afrika Mashariki katika tuzo za AFRIMMA 2021.

Katika kinyang’anyiro hicho Diamond alikuwa akishindanishwa na Ali Kiba kutoka Tanzania, Eddy Kenzo kutoka Uganda, Ben kutoka Rwanda, Khaligraph Jones kutoka Kenya, Gildo Kassa kutoka Ethiopia, Otile Brown kutoka Kenya na Meddy kutoka Rwanda.

Tuzo kwa mwanamuziki bora wa kike Afrika Mashariki imeenda kwa Faustina Mfinanga ‘Nandy’ ambapo alikuwa akishindanishwa na Nadia Mukami kutoka Kenya, Vinka kutoka Uganda, Zuchu kutoka Tanzania, Sheebah Karungi kutoka Uganda, Nikita Kering kutoka Kenya, Tanasha Donna kutoka Kenya na Knowles Butera kutoka Rwanda.

Kwa video bora ya mwaka ya AFRIMMA, ameshinda Flavour ft Diamond Platnumz x Fally Ipupa (Berna) ambapo alikuwa akishindanishwa na Tay C (Le Temps), Teni (Hustle), Mz Vee (Bosi Mbaya zaidi), Zuchu (Sukari), Ray Vanny x Innos’B (Kelebe), Rema (Bounce) na Wizkid ft Tems (Essence).

Mwongozaji bora wa Video ameshinda Director Kenny kutoka Tanzania ambapo alikuwa akishindanishwa na Dkt. Nkeng Stephens kutoka Cameroon, Deska Torres kutoka Kenya, TG Omori kutoka Nigeria, David Duncan kutoka Ghana, Sasha Vybz kutoka Uganda, Dammy Twitch kutoka Nigeria na Ofntse Mwase kutoka Afrika Kusini.