Simba kujenga uwanja wao, MO kuchangia bilioni 2

0
135

Klabu ya Simba imedhamiria kujenga uwanja wao utakaotumika na timu hiyo kama uwanja wa nyumbani.

Rais wa heshima na aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu hiyo, Mohamed Dewji (MO) ameandika kupitia ukurasa wake wa Twitter kuwa, amepokea maoni kutoka kwa Wanasimba wakishauri kujengwa kwa uwanja wa klabu hiyo na kwa kuanzia ameahidi kuchangia shilingi bilioni mbili, huku akiomba wanachama wachangie ujenzi huo.

Ameiomba Bodi ya Simba kuandaa utaratibu wa haraka ili jambo hilo lianze kutekelezwa.