Dkt. Salim atunukiwa tuzo ya heshima ya utatuzi wa migogoro

0
154

Rais Samia Suluhu Hassan amemkabidhi Waziri Mkuu
Mstaafu Dkt. Salim Ahmed Salim tuzo ya heshima ya utatuzi
wa migogoro, demokrasia na haki za binadamu, aliyotunukiwa na
taasisi ya Kemet Butros Ghali (KBG) ya nchini Misri.

Rais Samia amesema taasisi hiyo imempatia Dkt. Salim tuzo hiyo ili kuenzi mchango wake katika uongozi wa
Umoja wa Afrika kuanzia mwaka 1989 hadi 2001.

Sababu nyingine ni kutokana na Dkt. Salim kuonesha jitihada kubwa za kusaidia ukombozi wa nchi za Kusini mwa Afrika, kupigania haki, usawa, umoja, kudumisha ulinzi na usalama pamoja na kuleta maendeleo ya Afrika na dunia kwa ujumla.

Taasisi ya KBG imekuwa na utaratibu wa kutoa tuzo mbalimbali kila
mwaka na kutambua michango ya watu katika tafiti, elimu, amani,
demokrasia pamoja na kujishughulisha na masuala ya kuleta amani
na ujuzi.