Watu wanne wamefariki dunia na wengine 17 kujeruhiwa baada ya jengo la ghorofa moja lililokuwa likijengwa eneo la Goba kwa Awadhi mkoani Dar es Salaam kuporomoka.
Waliofariki ni wanaume wawili ambao walikuwa ni mafundi na wanawake wawili ambao walikuwa majirani.
Tayari mmiliki wa jengo hilo amekamatwa.