Ziara ya Rais Museveni Chato yaleta matunda

0
401

Tanzania kuendelea kushirikiana kwa ukaribu na Serikali ya Jamhuri ya Uganda katika kuimarisha mahusiano yaliyopo katika sekta za elimu biashara na uwekezaji kwa faida ya nchi hizo mbili

Rais Yoweri Museveni wa Uganda amemkabidhi Rais Samia Suluhu Hassan shule ya msingi na awali iliyojengwa kwa ushirikiano mkubwa wa Serikali ya Uganda na Tanzania na shule hiyo kupewa jina la Museveni

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema Serikali ya Tanzania itahakikisha shule hiyo iliyojengwa kwa lengo la kuimarisha ushirikiano katika sekta ya elimu unaendelea kuimarika na kuvutia wanafunzi wengi kutoka ndani na nje ya nchi

Rais Yoweri Museveni yupo nchini Tanzania kwa ziara ya siku 3 na leo hii akiwa Chato mkoani Geita amekabidhi shule hiyo kwa serikali ya Tanzania na kuridhia kupewa jina lake