Baadhi ya watu huzaliwa na tatizo la kutokuona rangi kabisa unaojulikana kisayansi kama achromatopsia. Japo wanakuwa na uwezo wa kuona kila kitu bila kujua ni cha rangi gani.
Tatizo hilo husababishwa na jenetiki na huweza kurithiwa kutoka kwa mzazi kwenda kwa mtoto.
Neil Harbisson wa Uingereza ni moja kati ya watu waliozaliwa na tatizo hilo. Kwa kipindi cha miaka 21 Neil hakuwahi kuona rangi na akiwa na miaka 21 alipata kifaa kama jicho la tatu anachovaa kichwani na kuning’inia usoni kinachomsaidia kujua rangi.
Kwa kutumia kifaa hicho Harbisson anapokuwa karibu na kitu kichaa hicho huweza kunasa mawimbi ya rangi ya kitu mbele yake, kupeleka mawimbi hayo mwilini na kisha kila rangi kutoa sauti mbalimbali ambazo kwa sasa Neil anazijua na kwa kusikia sauti hizo anaweza kutambua ni rangi gani ipo mbele yake.
Ameelezea tatizo hilo alilonalo wakati akizungumza katika kipindi cha TED.
Harbisson (37) anajishughulisha na utengenezaji wa vifaa vya kusaidia watu wenye tatizo kama lake na alishawishika kufanya hivyo baada kuchoka kuvaa.
Baada ya kuchoka kuvaa vifaa vikubwa vyenye uwezo huo na kutaka kifaa ambacho kitakuwa sehemu ya kiungo cha mwili.
Anasema sasa ameweza kupendelea rangi kadhaa tofauti na nyingine na kuwa na rangi anayopenda zaidi ‘favourite colour’.
Tatizo la achromatopsia hadi sasa halina tiba.