Dkt. Mwinyi: Zanzibar inajivunia mafanikio makubwa yaliyopatikana ndani ya miaka 60

0
263

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Mwinyi amesema ndani ya miaka 60 tangu kupatikana kwa Uhuru wa Tanzania Bara, kumekuwa na mafanikio makubwa na kubadili maisha ya wananchi wa Zanzibar.

Dkt. Mwinyi amesema hayo wakati wa mahojiano maalamu katika kipindi cha Mizani cha TBC kinachoongozwa na Dkt. Ayub Rioba Chacha kilichokuwa kikiangazia mwaka mmoja wa Rais Mwinyi tangu aingie madarakani.

“Nawapongeza watanzania kwa kudumisha amani ndani ya miaka 60 ya Uhuru, maendeleo yaliyopatikana ndani ya kipindi hiki ni makubwa sana.” -Rais Dkt. Mwinyi

Katika mahojiano hayo Rais Mwinyi amesema ndani ya mwaka mmoja wa uongozi wake, Zanzibar imefanikiwa kusimamia mapato bandari ya Zanzibar na kuongeza mapato hayo kwa kiwango kikubwa.

“Lazima tuongeze makusanyo ili tupate mapato, bandari ya Zanzibar ilikuwa ikipata shilingi bilioni 4 kwa mwaka na baada ya kuimarisha makusanyo hivi sasa makusanyo ni billioni 2.5 kwa mwezi.”- ameongeza Rais Dkt. Mwinyi

Janga la UVIKO-19 limetetemesha Dunia ikiwepo Zanzibar na kuifanya kushuka kiuchumi hivyo Serikali ya Zanzibar imekusudia kuingiza bilioni 460 ili kuimarisha uchumi wake.