Rais Samia aagiza ujenzi wa njia za waenda kwa miguu na baiskeli

0
259

Rais Samia Suluhu Hassan ameitaka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kuhakikisha wanajenga njia za waenda kwa miguu na waendesha baskeli katika barabara wanazojenga na watakazojenga.

Amesema kuwa lengo la serikali ni kupunguza uzalishaji wa moshi (hewa ukaa), hivyo badala ya wizara kujikita tu katika ujenzi wa reli, lazima waweke miundombinu rafiki ya watu kutembea na kuendesha baiskeli kwani kufanya hivyo hakuzalishi moshi.

Ametoa agizo hilo wakati akikagua mabanda ya wadau wa usalama barabarani katika ufunguzi wa Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani jijini Arusha.

Amesema hali ilivyo sasa hairidhishi kwani baiskeli, pikipiki na waenda kwa miguu wanapita katikati ya barabara, jambo ambalo linasababisha ajali zinazopelekea ulemavu na vifo.