Utoaji vibali vya uchimbaji madini wasitishwa

0
250

Rais Felix Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ametangaza kusitisha utoaji wa vibali vya uchimbaji wa madini nchini humo hadi hapo ofisi ya Msajili wa Madini ya nchi hiyo itakapofanya ukaguzi wa mahesabu ya fedha kwa kampuni za uchimbaji wa madini.
 
Ukaguzi huo unafanyika ili kudhibiti vitendo vya ubadhirifu na ufisadi katika sekta ya madini, vitendo ambavyo vinaelezwa kushamiri katika Jamhuri hiyo.
 
Hivi karibuni Waziri Mkuu wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo,  Augustin Matata Ponyo amefunguliwa mashtaka ya ubadhirifu wa fedha na ufisadi ambapo miongoni mwa mashtaka yanayomkabili ni kujipatia fedha kinyume cha sheria kupitia sekta ya madini.
 
Rais wa zamani wa nchi hiyo Joseph Kabila pia anatuhumiwa kujipatia fedha kwa njia za ufisadi yeye na familia yake pamoja na wasaidizi wa karibu yake.