Kigoma ni Mkoa wa kimkakati katika maendeleo- Katibu Mkuu CCM

0
135

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo amesema mkoa wa Kigoma ni kati ya mikoa maalumu ambayo serikali ya awamu ya sita inakusudia kuhakikisha maendeleo yake yanakwenda kwa kasi zaidi.

Akizungumza mara baada ya kuwasili mkoani humo kwa ziara ya Kikazi ya siku tatu, Chongolo pamoja na mambo mengine ame eleza kuguswa na juhudi zinazofanywa na serikali kufungua mkoa huo katika sekta ya miundombinu hususani barabara,anga na reli.

Amesema kwa sasa barabara zote za mkoa huo zinapitika vizuri na wakandarasi wapo kazini kuhakikisha maeneo yaliyobaki yanawekwa lami

Aidha ameipongeza serikali ya awamu ya sita kwa kutenga fedha nyingi kuimarisha sekta za afya na elimu mkoani humo na kusisitiza juhudi hizo kuendelezwa kwa kishindo.

Mapema akizungumza katika kijiji cha Kanyonza wilayani Kakonko Naibu Katibu Mkuu CCM Bara, Christina Mndeme amewataka wakazi wa mkoa huo kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali kwa kufanya Kazi Ili kuharakisha maendeleo ya nchi.