Balozi Mavura kuendeleza Diplomasia ya Uchumi

Ushirikiano wa Kimataifa

0
268

Tanzania na Korea Kusini kuendelea kushirikiana na kuimarisha fursa zilizopo kwa maendeleo ya kiuchumi, kiutamaduni na kijamii kwa wananchi wa mataifa yote mawili

Akizungumza jijini Seoul baada ya kuanza majukumu yake ya Ubalozi wa Tanzania nchini Korea Kusini Balozi Togolani Mavura amesema kazi iliyopo mbele yake ni kuendeleza diplomasia ya uchumi baina ya Mataifa hayo mawili

Balozi Togolani Mavura ni mmoja kati ya Mabalozi vijana wenye uzoefu na masuala ya ushirikiano wa kimataifa na diplomasia walioteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan na kuapishwa September 27 kuwa Balozi wa Tanzania nchini Korea Kusini