Timu zilizofuzu Kombe la Dunia mpaka sasa

0
229

Safari ya kwenda Qatar 2022 kwa ajili ya fainali za kombe la dunia imewadia, kwa timu zitakazoshiriki michuano hiyo kujulikana wiki hii, zile zitakazofungasha virago na zile zilizo kwenye hati hati, mguu ndani mguu nje zitajulikana pia.
Kwa upande wa Ulaya, washindi wa makundi wanakwenda moja kwa moja kwenye fainali hizo, ambazo zitapigwa kati ya Novemba 21 na Disemba 18, 2022.

Mashidano ya Qatar yatakuwa ya mwisho kushirikisha timu 32, kwa sababu idadi ya timu zimeongezwa mpaka 48 kuanzia fainali za mwaka 2026 zitakazofayika katika nchi za Marekani, Mexico na Canada.

Qatar, itashiriki mashindano haya kwa mara ya kwanza kabisa, NA imefuzu kama mwenyeji, ikitarajiwa kuwa timu ya kawaida katika fainali hizo.

Hizi ndio timu ambazo zimeshajihakikishia nafasi ya kushiriki michuano yatakayofanyika Qatar 2022.

  1. Ujerumani
  2. Ufaransa
  3. Ubelgiji
  4. Croatia
  5. Hispania
  6. Serbia
  7. Switzeland
  8. England
  9. Denmark