TPDC Kufanya biashara ya mafuta

0
184

Katika kukabiliana na changamoto ya mfumuko wa bei ya mafuta nchini Serikali inakuja na utaratibu wa kufanya biashara ya nishati hiyo kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio wakati wa semina ya Waandishi wa Habari ilivyoandaliwa na shirika hilo kuwajengea uelewa namna ya kuripoti habari za gesi na mafuta.

Aidha, Dkt. Mataragio amesema TPDC imeendelea kuzalisha sesi asilia inayotumika majumbani, viwandani na magari ambapo watumiaji wameendelea kuunganishiwa nishati hiyo.

Kuhusu kuzingatia usalama kwa watumiaji wa gesi asilia Dkt. Mtaragio amesema Serikali inaendelea kutoa elimu kuhusu matumizi ya nishati hiyo na kuongeza kuwa gesi hiyo ni salama na ikitokea mtungi ukavuja hewa husambaa hewani bila ya kuleta madhara kwa mtumiaji.