Dkt. Mwinyi mwaka mmoja madarakani

0
163

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi amewataka wawekezaji wanaowekeza Zanzibar kuhakikisha miradi wanayoitekeleza inawanufaisha wananchi wanaoishi karibu na miradi hiyo.
 
Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo kwa nyakati tofauti wakati akiweka mawe ya msingi katika ujenzi wa hoteli mpya ya kisasa ya Riu Jambo iliyopo Nungwi pamoja na hoteli ya Emerald Zanzibar Resort and SPA iliyopo Matemwe Mbuyuni mkoa wa Kaskazini Unguja, ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za kutimiza mwaka mmoja tangu aingie madarakani.
 
Amesema ni vema miradi inayotekelezwa iwe inawanufaisha wananchi kwa kupata ajira pamoja na kuuza bidhaa zao.
 
Rais Dkt. Mwinyi pia amewataka wawekezaji hao kuzifahamu changamoto zinazoikabili jamii katika maeneo yenye miradi yao,  ili wasaidie katika sekta mbalimbali ikiwa ni pamoja na elimu, afya na maji.