Balozi wa Msumbiji nchini Tanzania, Ricardo Mutumbuida amependekeza kuwepo kwa ushirikiano kati ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) na Televisheni ya Taifa ya Msumbiji ili kubadilishana uzoefu katika kuhabarisha umma.
Mutumbuida amesema hayo baada ya kutembelea studio za TBC zilizopo Barabara ya Nyerere, Dar es Salaam kujionea historia ya shirika hilo katika ukombozi wa Afrika kwa wakati huo ikifahamika kama Radio Tanzania Dar es salaam (RTD).

Naye Mkurugenzi wa Huduma za Redio, Aisha Dachi amesema kuwa TBC imejipanga vema kushirikiana na Shirika la Utangazaji Msumbiji, katika kubadilisha maudhui hasa ya ukombozi wa nchi hizo.
Balozi Mutumbuida ameipongeza TBC kwa kutunza historia za waasisi wa bara la Afrika.
