Wanaokwamisha miradi ya maji kufichuliwa

0
130

Mkuu wa wilaya ya Kigoma, Ester Mahawe ameuagiza Wakala wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijiji (RUWASA) kuwafichua Wenyeviti wa vijiji ambao wamekuwa wakikwamisha utekelezaji wa miradi ya maji kwenye maeneo yao.

Mahawe ametoa agizo hilo wakati wa mkutano wa nusu mwaka wa RUWASA wilayani Kigoma.

Amedai kuwa zipo taarifa kuwa kuna miradi ya maji imeshindwa kutekelezwa kwenye baadhi ya vijiji kutokana na Wenyeviti wa vijiji hivyo kutanguliza maslahi binafsi.

Aidha Mkuu huyo wa wilaya ya Kigoma amewataka wakazi wa wilaya hiyo kutunza miradi ya maji inayotekelezwa kwenye maeneo yao, Ili iwe endelevu kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.