Rais Samia kuunguruma Glasgow

0
298

Rais Samia Suluhu Hassan leo anatarajiwa kuhutubia
mkutano wa wakuu wa nchi wanaoshiriki katika mkutano wa 26 wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya Tabianchi (COP 26) unaofanyika Glasgow, Scotland.

Hapo jana Rais Samia Suluhu Hassan alihudhuria ufunguzi rasmi wa mkutano huo, ambapo Viongozi mbalimbali walipata fursa ya kuhutubia.

Mara baada ya ufunguzi rasmi wa COP 26, Rais Samia Suluhu Hassan alipata fursa ya kuhutubia moja ya mikutano maalum uliotishwa na Mawaziri Wakuu wa Uingereza na Italia pembezoni mwa mkutano huo wa Wakuu wa Nchi kuhusu mabadiliko ya Tabianchi uliopewa jina la Action and Solidarity, The Critical Decade Event.

Akihutubia mkutano huo, Rais Samia Suluhu Hassan ameeleza jitihada zinazofanywa na Serikali ya Tanzania katika kuhakikisha inakabiliana na mabadiliko ya Tabianchi ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua madhubuti kwenye sekta mbalimbali ikiwa ni pamoja na nishati, misitu na usafirishaji.