Tani elfu 33 za makaa ya mawe kusafirishwa kwenda India

0
145

Kwa mara ya kwanza bandari ya Mtwara imepokea meli kubwa ambayo itasafirisha tani elfu 33 za makaa ya mawe kwenda nchini India.

Meneja wa bandari ya Mtwara Mhandisi Juma Kijavara amesema makaa hayo ya mawe yamesafirishwa kwa malori kutoka mkoani Ruvuma na kampuni ya uchimbaji ya mkoani humo.

Kwa upande wake, mkuu wa mkoa wa Mtwara Brigadia Jenerali Marco Gaguti amesema uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali katika bandari ya Mtwara umeanza kuzaa matunda.

Amesema meli nyingi zinatarajiwa kufika katika bandari hiyo ya Mtwara kwa ajili ya kupeleka na kisafirisha bidhaa mbalimbali kwenda nje ya nchi.