Shule kufunguliwa tena baada ya miaka miwili nchini Uganda

0
319

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni ametangaza kuwa shule zitafunguliwa tena mwezi Januari 2022, takribani miaka miwili tangu kufungwa kutokana na mlipuko wa UVIKO-19.

Rais Museveni amesema hili litafanyika bila kujali wangapi wamechanja chanjo.

Chini ya 10% ya idadi ya watu nchini Uganda wamepokea chanjo, ingawa Rais Museveni amesema kutakuwa na chanjo za kutosha kabla ya mwisho wa mwaka.

Nchini Uganda wapo waalimu walioacha kazi ya ualimu na kutafuta kazi zingine na wengine wamedai Kuwa hawatarudi kazini