Binti Mfalme wa Japan azua gumzo

0
278

Mpwa wa Mfalme wa Japan Princess Mako ameamua kuachia hadhi yake ya kifalme ili aolewe na mwanaume ambaye ni raia wa kawaida waliokutana miaka 10 iliyopita wakiwa masomoni

Chini ya Sheria za Japan Mwanamfalme hunyang’anywa mamlaka na hadhi za kifalme anapoolewa na mtu wa kawaida ingawa wanafamilia wa kiume hawapotezi hadhi hizo

Mako anakuwa mwanamfalme wa kwanza wa familia ya ufalme huo wa Japan kukataa hayo yote na kuhamia katika penzi la Kei Komuro

Wawili hao wanapanga kuhamia nchini Marekani ambako Komuro anafanya kazi kama wakili huku tukio hilo likikumbusha tukio la wanafamilia ya Ufalme wa Uingereza Mwanamfalme Harry na mkewe Meghan Markle na kupewa majina bandia ya Japan’s Harry and Meghan