Wanajeshi wajaribu kuipindua serikali ya Sudan

0
358

Watu 12 wamejeruhiwa kufuatia mvutano kati ya waandamanaji na jeshi la Sudan, kufuatia uwepo wa jaribio la mapinduzi ya kijeshi lililoripotiwa leo alfajiri.

Waziri Mkuu wa Sudan, Abdalla Hamdok ni miongoni mwa viongozi wa kiraia walioripotiwa kuwa wamewekwa chini ya ulinzi (house arrest) na wanajeshi ambao hawajatambulika.

Kumekuwepo maandamano katika mji mkuu Khartoum, kufuatia baadhi ya watu kukamatwa na wanajeshi wenye silaha kali kuwepo mitaani.

Wizara ya Habari nchini humo mapema leo imesema kwamba wanajeshi wamewapiga risasi waandamani karibu na makao makuu ya wizara ya ulinzi.

Jumuiya za kimataifa zimetaka viongozi wa nchi hiyo kurejea kwenye mstari na kuhakikisha muda wa kurejesha utawala wa kiraia unabaki kama ulivyopangwa.