Rais Ndayishimiye aanza ziara nchini

0
176

Rais wa Jamhuri ya Burundi, Evariste Ndayishimiye, amewasili nchini leo kwa ziara ya Kitaifa ya siku tatu..

Akiwa nchini pamoja na mambo mengine, leo atatembelea na kuweka jiwe la msingi katika kiwanda cha kuzalisha mbolea ya asili yenye mchanganyiko wa madini ya phosphate na samadi kinachojengwa Dodoma. Kiwanda ambacho kinajengwa na Wawekezaji wa kampuni ya Itracom Fertilizers Limited (ITRACOM) kutoka nchini Burundi.

Oktoba 23, 2021 Rais Ndayishimiye ataelekea Zanzibar ambako atapokelewa na Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi na kuwa na mazungumzo na mwenyeji wake huyo na baadaye ataelelekea mkoani Dar es Salaam ambapo ataungana na mwenyeji wake, Rais Samia Suluhu Hassan.

Akiwa jijini Dar es Salaam Rais Ndayishimiye anatarajiwa kutembelea Bandari ya Dar es Salaam na kukagua ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) unaoendelea nchini kutokea stesheni ya Dar es salaam hadi stesheni ya Kwala – Ruvu mkoani Pwani, pamoja na kutembelea Bandari Kavu ya Kwala inayojengwa na Mamlaka ya Bandari Tanzania katika eneo hilo ili kujionea maendeleo ya ujenzi wa bandari hiyo.

TBCOnline #TBCUpdates #Aridhio #Burundi #Tanzania #Dodoma