Kina Sabaya kukata rufaa

0
353

Aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro Lengai Ole Sabaya na wenzake, leo wamewasilisha taarifa ya kusudio la kukata rufaa katika mahakama Kuu Kanda ya Arusha ya kupinga hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha tarehe 15 mwezi huu.
 
Wakili wa Sabaya, Moses Mahuna amesema kuwa baada ya kuwasilisha taarifa ya kusudio hilo la kukata rufaa, taratibu nyingine zinaendelea.
 
Sabaya na wenzake watatu wamehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha.
 
Hukumu hiyo ilitolewa baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kuridhika kuwa upande wa mashtaka umethibitisha mashtaka dhidi ya Sabaya na wenzake.