Hatma ya Mbowe leo.

0
218

Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu leo Oktoba 20, 2021 inatarajia kutoa uamuzi ya kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe na wenzake watatu.

Uamuzi wa kesi hiyo ulikiwa utolewe Oktoba 19 mwaka huu lakini kutokakana na Sikuu ya Maulid ikalazimu mahakama kusogeza mbele shuari hilo.

Hatua hiyo inakuja baada ya mahakama kupokea ushahidi wa mashahidi watatu wa upande wa mashtaka ukiongozwa na Wakili Serikali Mwandamizi Robaert Kidando na upande wa utetezi ukiongozwa na Wakili Peter Kibatala.

Kesi hiyo ndogo inahusiana na uhalali wa maelezo yaliyochukuliwa na Polisi kwa mshtakiwa wa pili Adamu Kasekwa, ambapo mawakili wa utetezi waliyapinga yasipokelewe kama kielelezo cha ushahidi wa upande wa mashtaka.

Upande wa utetezi uliyapinga maelezo hayo yasipokelewe kama kilelezo kwa madai kuwa yametolewa nje ya muda wa kisheria na kwamba mshtakiwa huyo pia hakuyatoa kwa ridhaa yake na pia wakati wa kuchukuliwa maelezo hayo alitishiwa na kuteswa.

Awali, katika hali isiyotarajiwa washitakiwa Freeman Mbowe na wenzake watatu kabla kuingizwa katika chumba cha mahakama baada ya kufikishwa mahakamani hapo na Jeshi la Magereza, mawakili wa utetezi wakiongozwa na Peter Kibatala walifanya maombi maalum juu ya shauri hilo.

Uamuzi wa kesi hiyo ndogo unatarajiwa kutolewa na Jaji Kiongozi wa mahakama hiyo Mustapha Siyani