Katika kuhakikisha sekta ya utalii inakua zaidi, Rais Samia Suluhu Hassan amesema serikali ipo tayari kutoa vibali kwa wawekezaji vya ujenzi wa hoteli za nyota tano, ili watalii waongezeke kutembelea vivutio mbalimbali vilivyopo nchini.
“Tunajitayarisha na ujenzi wa (Ma)toteli ya nyota tano, tumepokea wawekezaji kadhaa ambao wako tayari kujenga (Ma)hoteli mazuri ambayo wenzetu watajiskia raha kuyafikia na tupo njiani kutoa hivyo vibali ili mahoteli hayo yajengwe na wageni watakapo miminika kwetu wakute tuko tayari kuwapokea,”- Rais Samia Suluhu Hassan.