Rais Samia Suluhu Hassan ameeleza sababu za kusafiri nje ya nchi na kusema kuwa, anafanya hivyo ili kuendeleza mshikamano na mataifa mbalimbali rafiki.
“Ziara nilizokuwa nafanya nchi jirani zilikuwa na lengo la kuondosha vikwazo, tumeondosha vikwazo na Kenya na biashara imekuwa mara sita zaidi ya ilivyokuwa, kwahiyo tukizunguka msiseme mama anazunguka tu, sitozunguka bila sababu , nilishacheza vya kutosha kwenye nchi nyingi Duniani sasa hivi kazi ni moja tu kuzunguka kwa ajili ya maendeleo ya Tanzania,”- Rais Samia Suluhu Hassan.