Ajali yaua mmoja Katavi

0
278

Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Iddi Mande amefariki dunia na wengine watano kujeruhiwa katika ajali ya basi la abiria mali ya Kampuni ya Adventure lililokuwa likitoka Mpanda kuelekea mkoani Kigoma.

Kamanda wa polisi mkoa wa Kigoma, Kamishna Msaidizi, James Manyama amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo katika eneo la Maghorofani wilayani Uvinza na kusema kuwa basi hilo lililokuwa na abiria 65 limepinduka baada ya tairi la mbele kupasuka .

Aidha, Kamanda Manyama amesema majeruhi wa ajali hiyo wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma, Maweni na wengine katika kituo cha afya cha Uvinza na kwamba wanaendelea vizuri.

Kufuatia tukio hilo jeshi hilo mkoani Kigoma limewataka madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani ikiwemo kuepuka kuendesha vyombo vya moto kwa mwendokasi .