Profesa Mbarawa aagiza ujenzi ukamilike haraka

0
130

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa ametoa muda wa miezi minne kwa mkandarasi Chico Construction,  kukamilisha ujenzi wa barabara ya Tanga – Pangani.
 
Waziri Mbarawa ametoa muda huo mara baada kutembelea barabara hiyo na kujionea ujenzi unavyoendelea.
 
Amemtaka mkandarasi huyo ashirikiane na Watendaji wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) pamoja na wale wa mkoa wa Tanga ili kukamilisha ujenzi wa barabara hiyo katika kipindi alichoagiza.
 
Barabara ya Tanga – Pangani yenye urefu wa kilomita 50 inajengwa kwa kiwango cha lami, ambapo mkataba wa ujenzi huo ulisaini Julai 31 mwaka 2019 kati ya Serikali ya Tanzania na mkandarasi huyo ambaye ni Chico Construction.