Dkt. Gwajima kumwakilisha Rais Russia

0
116

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima anatarajiwa kumwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika kongamano la tatu la Kimataifa la Wanawake,  litakalofanyika nchini Russia kwa muda siku tatu kuanzia tarehe 13 mwezi huu.
 
Akiwa katika kongamano hilo, Dkt. Gwajima ataonesha namna Tanzania ilivyofanikiwa katika kuwa na usawa wa kijinsia, kuwainua Wanawake kiuchumi na kutambua mchango wao katika maendeleo ya Taifa.
 
Dkt. Gwajima anashiriki katika kongamano hilo ikiwa ni mwelekeo na azma ya Serikali ya awamu ya sita katika kuhakikisha uwepo wa usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa Wanawake katika nyanja mbalimbali.
 
Lengo la kongamano hilo la tatu la kimataifa la Wanawake ni kutambua mchango wa Wanawake katika maendeleo ya Dunia,  kuonesha mchango wa Wanawake katika maendeleo na kuhakikisha kunakuwa na usawa wa kijinsia.
 
Kongamano hilo linashirikisha Viongozi kutoka mataifa mbalimbali, mashirika yasiyo ya Kiserikali, Wabunge, Mashirika ya Kimataifa, Wakuu wa mitandao ya kimataifa ya Wanawake na wawakilishi wa kampuni za biashara duniani.