Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichoka amesema Serikali imejipanga kuboresha Mfumo wa Mitaala ya Elimu ya Juu Nchini ili kuzalisha Wanafunzi wenye Ujuzi Shindani itakayoleta mageuzi ya kiuchumi kwa Taifa.
Akizungumzia Hatua Hiyo jijini Dar es Salaam amesema tayari Serikali imesaini mkataba wa mradi unaofadhiliwa na Benki ya Dunia shilingi bilioni 982 kwa ajili ya kuendeleza sekta ya elimu ya juu nchini .
Kwa upande wake Mjumbe wa Kamati ya Usimamizi wa Mradi Prof. Dominic Kambarage amesema mradi huo ni wa pekee nchini huku Makamu wa Chuo Kikuu cha Dodoma Prof. Fautine Bee akisema mradi huo utaboresha miundombinu ya chuo na taaluma kwa jumla.
