Dkt. Mwinyi akutana na viongozi wa Tawala za Mikoa

0
158

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.  Hussein Mwinyi ameeleza kutoridhishwa na utendaji kazi wa mamlaka za Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ikiwa ni pamoja na Mabaraza ya Miji, halmashauri na Manispaa za Zanzibar.

Dkt. Mwinyi ameyasema hayo alipokutana na Viongozi wote wa Serikali za Mitaa kutoka mikoa yote ya Zanzibar wakiwemo wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya zote za Unguja na Pemba, Ikulu jijini Zanzibar.

Amewataka wakuu wa mikoa na wilaya zote za Zanzibar kuhakikisha suala la ulinzi, amani na usalama katika maeneo yao linasimamiwa na kupewa kipaumbele.

Aidha, Rais Mwinyi amezitaka mamlaka za Manispaa na Mabaraza ya Miji kusimamia ukusanyaji wa mapato pamoja na matumizi yake, ili kuwaletea Wananchi maendeleo.