Tuzo za Rais za wazalishaji bora kutolewa Oktoba 8

0
5075

Shirikisho la wenye viwanda nchini CTI Kwa kushirikiana na
shirika la Maendeleo la Ujerumani GIZ wamewataka
Wazalishaji viwandani kuwa na utamaduni wa kushiriki na
kuwania Tuzo za Rais za Mzalishaji bora viwandani ili kusaidia
kuongeza ushindani wa uzalishaji wa bidhaa bora.

Hayo yameelezwa jijini Dar es Salaam, wakati wa kutangaza
Tarehe ya kutolewa kwa tuzo za Rais za wazalishaji bora
viwandani ambazo zinatarajiwa kutolewa oktoba 8 huku Mgeni
rasmi akitarajiwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania DKT PHILIP Mpango.

Akizungumza katika Mkutano na waandishi wa habari,
Mkurugenzi Mtendaji wa CTI LEODGAR TENGA amesema
takribani viwanda 78, vikiwemo vikubwa, vya kati na
vidogo katika sekta 24 ikiwemo za biashara, vinywaji na
huduma zimeshiriki kuwania tuzo hizo.

Tenga amesema, tuzo za mwaka huu zitakuwa na toauti kubwa kutokana na ushindani mkubwa kutoka kwa wazalishaji wa bidhaa mbalimbali hapa nchini.