Taiwan yaishutumu China kwa uchokozi

0
186

Taiwan imetangaza hali ya tahadhari kufuatia hatua ya China ya kuendelea kurusha ndege zake za kijeshi katika anga lake, hatua ambayo imeelezwa kuwa ni ya uchokozi.

Akitangaza hali hiyo ya tahadhari Waziri Mkuu wa Taiwan, Su Tseng – Chang amesema wataendelea kufuatilia kwa karibu hatua hiyo ya China ambayo amesema haivumiliki.

Amesema Taiwan itaendelea kulinda usalama wake ambapo ndege zake za kivita na mifumo ya kujihami ya makombora imewekwa katika hali ya tahadhari, ili kukabiliana na vitendo hivyo vya China ambavyo vimeelezwa kuendelea kwa siku ya tatu mfululizo.

Marekani ambayo ni mshirika wa karibu wa Taiwan imelaani hatua hiyo ya China, huku Japan ikizitaka China na Taiwan kumaliza mzozo huo kwa njia ya amani.

Kwa upande wake China k ambayo inadai Taiwan ni sehemu yake imesisitiza kisiwa hicho kitambue kuwa sio taifa kamili bali ni eneo lake.