Waraka wa siri waanika mali za viongozi

0
207

Mfalme Abdullah wa Pili wa Jordan ni miongoni mwa viongozi ambao wametajwa katika taarifa za siri zilizovuja ambazo zinaonyesha mali zinazomilikiwa kwa siri na viongozi hao.

Waraka huo wa taarifa za siri unaojulikana kama Pandora Papers unaonyesha kuwa Mfalme Abdullah wa Pili anamiliki mali za dola milioni mia moja za Kimarekani ambazo zimewekezwa kwa siri katika miji mbalimbali ikiwemo Malibu, California, Washington na London.

Viongozi wengine wanaotajwa katika waraka huo ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Czech – Andrej Babis ambaye anamiliki mali za thamani ya dola milioni 22 za Kimarekani ambazo zimewekezwa kwa siri Kusini mwa Ufaransa.

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya pia anatajwa katika waraka huo ambapo anadaiwa kumiliki mali za thamani ya dola milioni 30 za Kimarekani ambazo zimewekezwa kwa siri nchini Uingereza.