Manny Pacquiao kuwania urais

0
182

Bingwa wa zamani wa ndondi duniani Manny Pacquiao amewasilisha nyaraka za kuthibitsha kuwania urais wa Ufilipino, na hivyo kuwa mwanasiasa wa kwanza nchini humo kutangaza rasmi kwamba atagombea nafasi hiyo kwenye uchaguzi utakaofanyika mwaka 2022.
 
Pacquiao ambaye kwa sasa ni Seneta amesema, iwapo atashinda kiti hicho cha urais ataelekeza nguvu zake katika kupambana na umaskini na ufisadi pamoja na kushughulikia janga la UVIKO – 19.
 
Pamoja na kuwa mwanachama na mmoja wa viongozi katika chama tawala cha PDP –  Laban  kinachoongozwa na Rais  wa sasa wa Ufilipino, Rodrigo Duterte, Pacquiao anagombea kiti cha urais kupitia chama chake cha People’s Champ Movement kufuatia mvutano baina yake na Duterte.