Kanali Mamady Doumbouya ameapishwa kuwa Rais wa mpito wa Guinea, baada ya kuongoza mapinduzi ya kijeshi yaliyomuondoa madarakani Rais Alpha Condé wa nchi hiyo mwezi Septemba mwaka huu.
Kanali Doumbouya mwenye umri wa miaka 41 anakuwa Rais wa pili barani Afrika kwa kuwa na umri mdogo, huku Rais mwenye umri mdogo kuliko wote akitajwa kuwa ni Assimi Goïta wa Mali mwenye umri wa miaka 38 ambaye naye alichukua madaraka baada ya mapinduzi ya kijeshi..
Kanali Doumbouya ameapishwa kuwa Rais wa mpito zikiwa zimepita siku chache baada ya kuzuiwa kugombea kiti cha urais katika uchaguzi ujao.
Kwa mujibu wa masharti ya uchaguzi huo wa Urais, mtu yoyote atakayekuwa kiongozi katika serikali ya mpito, hataruhusiwa kugombea katika uchaguzi huo.